Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HABARI KUTOKA LIBYA ZASEMA WATU ZAIDI YA 400 WAFARIKI DUNIA BAADA YAKUZAMA MAJINI.

HABARI KUTOKA LIBYA ZASEMA WATU ZAIDI YA 400 WAFARIKI DUNIA BAADA YAKUZAMA MAJINI.

Written By Unknown on Wednesday 15 April 2015 | Wednesday, April 15, 2015

Wahamiaji haramu zaidi ya 400 wameaga dunia katika pwani ya Libya baada ya boti waliyokuwa wakisafria kuzama jana katika pwani hiyo. Askari wanaolinda pwani ya Italia awali walisema kuwa wamefanikiwa kuwaokoa wahamiaji haramu 144 na kupata miili kumi ya wahamiaji haramu waliozama na kisha kuipeleka hadi pwani. Shirika la habari la Ufaransa limeripoti kuwa, wahamiaji hao haramu waliozama ambao  wengi wao walikuwa ni kutoka nchi za Kiafrika na za eneo la Mashariki ya Kati walikuwa na lengo la kuingia Italia kinyume cha sheria kupitia Libya. Miezi kadhaa iliyopita pia, mamia ya wahamiaji haramu kutoka nchi za Kiafrika waliaga dunia wakiwa katika maji ya bahari ya Mediterania wakisafari kuelekea nchi za Ulaya.   

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi