Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » KAMA ULIKUA HAUJUI BASI HIKI NDICHO ALICHO KIFANYA MWANASOKA HUYU.

KAMA ULIKUA HAUJUI BASI HIKI NDICHO ALICHO KIFANYA MWANASOKA HUYU.

Written By Unknown on Wednesday 15 April 2015 | Wednesday, April 15, 2015

Mshambuliaji wa timu ya Chelsea F.C. Didier Drogba amezindua hospitali ya kwanza, kubwa na ya aina yake kati ya tano alizo wahi kuahidi kuzijenga kama sehemu ya kujitolea kwa jamii yake .
Hospitali hiyo iko wilaya ya Attécoubé katika mji wa kibiashara wa Abidjan, hospitali hiyo imemgharimu nguli huyo wa kandanda kiasi cha dola milioni moja za kimarekani ili kukamilisha mjengo huo wa afya ;na hospitali hiyo ni maalumu kwa wanawake na watoto wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu .
Hospitali hiyo imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba mia nane (800) huduma kadhaa zinapatikana ikiwamo chumba cha uchunguzi, wodi ya wazazi,kitengo cha watoto,jengo la x-ray ,jengo la kisasa la maabara,duka kubwa la dawa,jengo la kulaza wagonjwa na jengo tengefu la wagonjwa.
Inakadiriwa hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa elfu hamsini kwa mwaka na hii ni kwa muujibu wa katibu mkuu wa asasi ya Didier Drogba Foundation , Guy Roland Tanoh ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mradi huo.
Hospitali zingine nne zilizo katika ahadi za mwanasoka huyo ziko katika hatua za ujenzi za mwisho mwisho kukamilika ambazo ziko nchini Ivory Coast katika miji ya Yamoussoukro, San Pedro, Man na Korhogo na zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao.
Mshambuliaji huyo wa timu ya Chelsea na pia timu ya Elephants anabakia kuwa mchezaji na mfungaji bora na wa mfano wa kuigwa nchini mwake pamoja na kwamba amestaafu kuichezea timu yake ya taifa,ambayo iliutwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Africa mwaka huu nchini Equatorial Guinea mnamo mwezi wa February.Asasi hiyo ya Drogba foundation inaandaa chakula cha hisani mjini London mwezi huu wa April tarehe 18 ili kupata fedha za kukamilisha miradi hiyo.
Kazi nzuri Didier Drogba! .
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

1 comment:

  1. Best Casino Sites in Canada for 2021
    Find the best gambling sites in Canada today. Casino has 배당 토토 been on a steady 바카라사이트casinopan rise since it was launched back in 먹튀 랭크 2014. It offers 무료슬롯머신 over 550 games, 엠비 션 주소

    ReplyDelete

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi