Madaktari wakijiandaa kuanza kazi ya upasuaji. |
Kosa hilo kubwa mno limeigharimu hospitali hiyo Dola za Marekani 6,000 baada ya uchunguzi wa pamoja na ongezeko la faini ya Dola za Marekani 16,000 baada ya mgonjwa mwingine kuanguka na kuumia kichwani wakati alipotelekezwa bila kuhudumiwa mwaka 2011, kwa mujibu wa ripoti za gazeti la Syracuse Post-Standard.
Colleen S. Burns wa North Syracuse, mjini New York, mwenye umri wa miaka 41, alikuwa amelazwa hospitalini hapo Oktoba 2009 kwa tatizo la kujizidishia dozi ya dawa.
Sababu ya mfululizo wa makosa katika tathimini, madaktari waliamini kwamba mwanamke huyo alikuwa amekufa na kuanza mchakato wa kuchangisha viungo.
Uchunguzi wa Idara ya Taifa ya Afya kuhusu tukio hilo uligundua kwamba pale Burns alipolazwa kwanza, waliruka matibabu yaliyopendekezwa kwamba ingeweza kuzuia dawa hizo alizotumia - Xanax, Benadryl na zile za kulainisha misuli - zisifyonzwe na tumbo lake na matumbo.
Pia hawakufanya vipimo vya kutosha kuona kama hakuwa na dawa zilizobaki au kufanya kaguzi za kutosha kwenye ubongo.
Sababu hawakufanya kaguzi hizi za kutosha, madaktari waliamini kwamba ubongo wa Burns haukuwa ukifanya kazi, wakati uhalisia kujizidishia huko dozi kulimfanya azimie kwa muda mrefu.
Baada ya madaktari kusema ubongo wake ulikuwa haifanyi kazi, familia yake ilikubali kumwondoa kwenye mashine za kusaidia kupumua na viungo vyake kutolewa kwa ajili ya kuchangia wenye mahitaji.
Lakini siku hiyo kabla viungo hivyo havijaondolewa, muuguzi mmoja alifanya tendohiari na kugundua kwamba Burns alikuwa bado ana fahamu.
Alikunja vidole vyake chini ya moja ya miguu ya Burns na vidole vyake vya mguuni vikajikunja kwenda chini, ishara kwamba alikuwa angali hai.
Na hiyo haikuwa ishara pekee ya uhai. Wakati alipokuwa akipelekwa kwenye chumba cha upasuaji, matundu ya pua ya Burns yalikuwa yakicheza na kuonesha kwamba alikuwa akipumua mwenyewe kutoka kwenye kipumulio.
Pia midomo yake na ulimi navyo vilikuwa vikitikisika.
Lakini madaktari walipuuza ugunduzi wa muuguzi huyo ambao uliashiria kwamba Burns bado yuko hai, na wakaendelea na upasuaji bila kujali.
Kabla ya mchakato huo, Burns alikuwa amechomwa sindano ya kutuliza ya Ativan, lakini si kitulizo hicho au ugunduzi wa uhai uliorekodiwa kwenye karatasi ya daktari kwa ajili ya mchakato huo.
Haikuwa hivyo hadi Burns alipofumbua macho yake kwenye chumba cha upasuaji ndipo mchakato huo ulipositishwa.
Si Burns au familia yake iliyoishitaki hospitali hiyo kwa kuzembea kazi.
Miezi 16 baadaye, Burns akafanikiwa kujiua.
Mama yake, Lucille Kuss alisema binti yake hakuwa amefadhaishwa na tukio hilo.
"Alikuwa amehuzunishwa mno kwamba haikuwa imebadilisha chochote kwake," alisema Kuss.
Hospitali hiyo hata haikuripoti tukio hilo, wala kufanya uchunguzi wao binafsi.
Iliendelea hivyo hadi baada ya Post-Standard kuanza uchunguzi wao ambao hospitali hiyo hakutoa maelezo ya aina yoyote kwa kile kilichotokea.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!