|
. |
Katika
hali isiyo ya kawaida mamba mkubwa mwenye futi 8 amezua tafrani baada
ya kuingia chini ya kitanda cha Mkurugenzi wa hoteli moja ya kitalii
iitwayo Humani iliyopo pembezoni mwa mto Turgwe huko nchini Zimbabwe na
kukaa zaidi ya masaa 8.
|
. |
Mr
Whittall, ambaye ni mkurugenzi wa hoteli hiyo alisema kuwa mamba huyo
aliingia kwa siri chumbani kwake na kukaa chini ya kitanda chake usiku
na kugundulika asubuhi ya siku iliyofuata.
|
. |
Alisema
kuwa mamba huyo alitoka nyuma ya pori lililopo karibu na hoteli hiyo
ambapo hata yeye alipoamka hakumuona na alining’iniza miguu yake huku
mamba huyo akiwa chini ya kitanda ambapo alitoka kwenda kupata kifungua
kinywa kwenye mgahawa wa hoteli hiyo.
|
. |
Inaelezwa
kuwa mamba huyo aligundulika na mfanyakazi aliyekuwa akifanya usafi
katika chumba hicho na kupiga mayowe yaliyomshtua Mr Whittall ambapo
alitoka mbia kwenda kushuhudia kulikoni na kumkuta mamba huyo akiwa
chini ya kitanda chake kumbe alilala naye kwenye chumba hicho usiku
mzima.
|
. |
Mamba
ni wataalam wa kujificha na ndiyo maana hunusirika kuuwawa na wanyama
wengine hususani binadamu hata wakiwa nje ya maji,alisema Mr Whittall.
|
. |
Na
huweza kutulia sehemu moja kwa muda mrefu bila kugundulika na myama
yoyote hivyo kumtambua inakuwa ni vigumu hiyo ni kutokana na maumbile
yao yalivyo na hukimbilia ndani ya vichaka au kuingia kwenye nyumba kama
hotelini hapo kufuata joto hasa katika kipindi cha mvua na baridi kali
na alipenda kukaa chini ya kitanda hicho kwasababu kulikuwa na joto.
|
Mkurugenzi
huyo alilazimika kuwaita wafanyakazi wengine ambao walisaidiana
kumuondoa mamba huyo kutoka kwenye chini ya kitanda na kumtupa kwenye
bwawa la hoteli hiyo. |
|
. |
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!