CAPE VERDE YANYANG'ANYWA NAFASI KWA KUTUMIA MCHEZAJI MWENYE KADI.
NDOTO za Cape Verde
kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mwakani nchini
Brazil zilizimika ghafla baada ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA
kuwakuta na hatia ya kutumia mchezaji asiyeruhusiwa katika mojawapo ya
mechi zao za kufuzu. Nafasi
yao ya kwenda katika hatua ya mtoano inatarajiwa kuchukuliwa na Tunisia
ambao walienguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupewa kuchapo
cha mabao 2-0 wakiwa nyumbani kwao na Cape Verde. Kufuatia kipigo hicho kocha wa Tunisia Nabil Maaloul alijiuzulu wadhifa wake huo kutokana na kipigo hicho cha aibu. Katika
taarifa iliyotumwa katika mtandao wake FIFA ilidai kukuta Cape Verde na
makosa ya kumchezesha beki wao Fernando Varela ambaye alikuwa
akitumikia adhabu baada ya kutolewa nje katika mechi za kufuzu Machi
mwaka huu hivyo kuizawadia Tunisia ushindi wa mabao 3-0. Kwa
maana hiyo Tunisia inakua imemaliza mechi zake ikiwa inaongoza kundi B
na kuungana na washindi wa makundi mengine katika ratiba ya mwisho ya
hatua ya mtoano kabla ya timu tano kufuzu kwenda Brazil. Mbali na kuinyima ushindi Cape Verde kamati ya nidhamu ya FIFA pia iliitoza faini nchi hiyo ya dola 6,400.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!