Shirika la Msamaha Duniani Amnesty
International limekosoa hatua ya kuondolewa kwa nguvu makumi ya maelfu
ya watu wanaotafuta hifadhi kutoka katika kambi za mji mkuu wa Somalia,
Mogadishu. Amnesty imesema kuwa, hatua hiyo imesababisha vitendo vya
ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu vikiwemo vya mauaji na ubakaji.
Karibu Wasomali 370,000 wamekuwa wakiishi makambini mjini Mogadishu
kutokana na ukame, njaa na mapigano. Hata hivyo serikali ya Somalia hivi
karibuni ilianza mpango wa kuwahamishia wakimbizi hao wa ndani katika
kambi zilizoko nje ya Mogadishu suala ambalo limepingwa na wakimbizi hao
na kuleta mtafaruku mkubwa.
Amnesty International imesema kuwa,
mpango huo ungeweza kuwa na mafanikio makubwa iwapo wakati wa kuhamishwa
watu hao yangeheshimiwa pia mahitaji yao, haki zao na usalama wao.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!