KATIBU mkuu wa kamati ya
maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar
2022 Hassan al-Thawadi amepinga hoja ya michuano hiyo kuhamishiwa katika
nchi nyingine. Shirikisho
la Soka Dunia-FIFA katika kikao chake kijacho wanapanga kujaribu
kuhamisha michuano hiyo katika majira ya baridi ili kukwepa joto kali
katika kipindi cha kiangazi nchini Qatar. Mwenyekiti
wa Chama cha Soka cha Uingereza Greg Dyke amesema kuna uwezekano
michuano hiyo ikahamishiwa nchi nyingine kama muda mzuri wa kucheza
nchini Qatar hautakubaliwa. Lakini
kauli hiyo imeonekana kupingwa vikali na Al Thawadi akisisitiza kuwa
hakuna sababu ya kwanini Qatar isiandae michuano hiyo kama
ilivyopangwa. Al
Thawadi amesema walifanya kazi kubwa kuhakikisha wanakidhi viwango
katika kutafuta nafasi hiyo na muda huohuo kuhakikisha wanatimiza ahadi
walizotoa hivyo haoni sababu ya kuhamisha michuano hiyo mahali pengine.
Home »
michezo ulaya
,
news
» QATAR WAPINGA HOJA YA KUWANYANG'ANYA HAKI ZA KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2022.
QATAR WAPINGA HOJA YA KUWANYANG'ANYA HAKI ZA KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2022.
Written By Unknown on Friday, 13 September 2013 | Friday, September 13, 2013
Labels:
michezo ulaya,
news
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!