NGULI wa soka nchini
Brazil Pele, amedai kuwa timu ya taifa ya nchi hiyo haipaswi kumtegemea
mshambuliaji wake nyota Neymar moja kwa moja. Nyota
huyo amekuwa mshambuliaji tegemeo kwa Brazil toka ang’are katika
michuano ya Kombe la Shirikisho mapema mwaka huu huku akufunga mabao
tena katika mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Australia na
Ureno. Hata hivyo,
Pele anadhani hata kama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21
ameonyesha kukomaa haipaswi kumtwisha majukumu mengi kwani inaweza
kuigharimu nchi hiyo wakati watakapomkosa. Pele
amesema nchi hiyo ina vipaji vingi ambavyo kocha anaweza kuvitumia bila
ya kutegemea huduma ya mchezaji mmoja moja kwa moja.
BRAZIL HAIPASWI KUMTEGEMEA NEYMAR PEKEE - PELE.
Written By Unknown on Friday, 13 September 2013 | Friday, September 13, 2013
Labels:
michezo ulaya,
news
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!