KAMATI ya nidhamu ya
Shirikisho la Soka Duniani-FIFA imetupilia mbali madai yaliyotolewa na
Shirikisho la Soka la Congo wakidai kuwa Niger ilichezesha mchezaji
asiyeruhusiwa katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia baina ya timu hizo
Septemba 7 jijini Niamey. Hatua
hiyo ya FIFA inamaanisha kuwa Burkina Faso wanabakia kama viongozi wa
kundi E hivyo kufuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo. Maofisa
wa soka wa Congo wamedai kuwa Niger ilimtumia Mahamane Cisse ambaye
uraia wake ulikuwa na matata hivyo kumfanya kukosa vigezo vya kucheza
mechi hiyo. Hata hivyo FIFA walitupilia mbali madai hayo na kudai kuwa Niger hawakukiuka sheria zozote kwa kumtumia mchezaji huyo.
FIFA YAITOSA DRC.
Written By Unknown on Friday, 13 September 2013 | Friday, September 13, 2013
Labels:
michezo africa,
news
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!