Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
amesisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa ndio chombo pekee kinachopaswa kufuatilia mgogoro wa
Syria. Akizungumzia mabadiliko yanayojiri Syria, Zuma amesema, katika
mkutano wa kundi la G20 uliofanyika huko Petersburg nchini Russia nchi
nyingi hasa wanachama wa kundi la Bricks zilipinga mpango wa
kushambuliwa Syria. Zuma aidha ameongeza kuwa, Umoja wa Mataifa ndio
mahali bora zaidi pa kutatulia mgogoro wa Syria na masuala mengine
yanayohusu usalama wa dunia.
Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi duniani zilizopinga waziwazi hatua ya Marekani ya kutaka kuishambulia kijeshi Syria.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!