SERIKALI ya Ivory Coast imetangaza kutafuta nafasi ya kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2019 au 2021. Kwa
wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka la nchi hiyo-Fecafoot,
imedai kuwa serikali imewaruhusu kutuma barua ya maombi kwa Shirikisho
la Soka barani Afrika-CAF. Ili
kuhakikisha wanapata nafasi ya kuandaa michuano hiyo serikali ya nchi
hiyo imepanga kutengeneza mazingira rafiki ikiwemo suala la kuboresha
miundo mbinu yake. Mara
ya mwisho Ivory Coast kupata uenyeji wa kuandaa michuano hiyo ilikuwa
mwaka 1984 lakini harakati zao za kutaka kuandaa michuano ya mwaka 2006
ziligongwa mwamba kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyokuwepo nchini
humo.
IVORY COAST KUTAFUTA NAFASI YA KUANDAA AFCON 2019 AU 2021.
Written By Unknown on Friday, 13 September 2013 | Friday, September 13, 2013
Labels:
michezo africa,
news
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!