Zain al Abideen bin Ali dikteta wa zamani wa Tunisia, ameteuliwa kuwa mshauri wa mwanamfalme Bandar bin Sultan, Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Saudi Arabia.
Dikteta huyo wa zamani wa Tunisia ambaye alikuwa kibaraka wa Magharibi, alikimbilia na kupewa hifadhi nchini Saudi Arabia baada ya wananchi na wanaharakati wa Tunisia kumng'oa madarakani mwaka 2011.
Bandar bin Sultan anatuhumiwa kuwa anaongoza na kuyasaidia kifedha na kwa silaha makundi ya kigaidi nchini Syria. Imeelezwa kuwa, dikteta wa zamani wa Tunisia baada ya kukimbilia nchini Saudi Arabia pamoja na familia yake aliishi kwa muda wa mwaka mmoja mjini Jeddah kwenye kasri la kifalme la Fahd bin Abdulaziz, mfalme wa zamani wa nchi hiyo na kisha akaelekea kwenye mji wa Abha ulioko umbali wa kilomita 450 kusini mwa mji wa Jeddah.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!