Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » Hatma ya watuhumiwa wanne wa ubakaji nchini India kujulikana leo

Hatma ya watuhumiwa wanne wa ubakaji nchini India kujulikana leo

Written By Unknown on Friday, 13 September 2013 | Friday, September 13, 2013

Waandamanji nchini India wakiwa na mabango kupinga vitendo vya ubakaji na kushinikiza adhabu kali dhidi ya watuhumiwa
Waandamanji nchini India wakiwa na mabango kupinga vitendo vya ubakaji na kushinikiza adhabu kali dhidi ya watuhumiwa

Watuhumiwa wanne wa ubakaji nchini India hii leo watajua hatma yao wakati huu majaji wa mahakama kuu mjini New Delhi wakijiandaa kutoa hukumu inayosubiriwa kwa hamu na wananchi.

Siku tatu zilizopita watuhumiwa wote wanne walipatikana na hatia ya makosa ya ubakaji, mauaji na utekaji nyara ambapo majaji walitangaza siku ya Ijumaa kuwa watasoma adhabu inayowakabili watu hao.
Mwendesha mashtaka kwenye kesi hiyo ameiomba mahakama kutoa adhabu ya kifo dhidi ya watuhumiwa hao wanne kutokana na makosa yenyewe ambayo wametenda ingawa adhabu ya juu nchini India ni kifungo cha maisha gerezani.
Jaji Yogesh Khanna ndiye atakayesoma hukumu hiyo ambapo awali anatarajiwa kufafanua iwapo watuhumiwa hao wanne wanastahili adhabu ya juu kabisa ya kunyongwa au la.
Tayari maelfu ya wanaharakati na wananchi wamefurika nje ya mahakama ambako hukumu hiyo itatolewa wakiwa na mabango kuwashinikiza majaji kutoa adhabu ya kifo kwa watuhumiwa hao.
Mtuhumiwa mmoja kati ya hao ambaye alikuwa dereva wa basi ambalo watuhumiwa hao walishirikiana kutekeleza kitendo hicho alikutwa amejinyonga kwenye chumba chake cha mahabusu huku mtuhumiwa mwingine akihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi