Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » Serikali ya mpito nchini Misri yatangaza kuongeza muda zaidi wa hali ya hatari

Serikali ya mpito nchini Misri yatangaza kuongeza muda zaidi wa hali ya hatari

Written By Unknown on Friday, 13 September 2013 | Friday, September 13, 2013

Rais wa mpito wa Misri, Adly Mansour
Rais wa mpito wa Misri, Adly Mansour

Serikali ya mpito nchini Misri, imetangaza kuongeza muda wa hali ya hatari nchini humo kwa miezi miwili zaidi kufuatia ule muda wa awali kumalizika, huku jeshi likidai ni kutokana na sababu za kiusalama.

Uamuzi wa kuongeza muda huo umetangazwa na rais wa Serikali ya mpito ya Misri, Adly Mansour ambaye amesema kutokana na sababu za kiusalama wamelazimika kuongeza muda zaidi wa hali ya hatari mpaka pale watakapojiridhisha kuwa usalama umerejea.
Uamuzi huu unakuja huku ule muda wa mwezi mmoja uliokuwa umetengwa hapo awali ukikaribia kumalizika huku operesheni za kuwakamata viongozi wa juu wa Muslim Brotherhood ikiendelea.
Serikali ya mpito ya Misri iliamua kutangaza hali ya hatari nchini humo kufuatia maandamano yaliyoshuhudia watu zaidi ya elfu moja wakipoteza maisha kutokana na makabiliano ya raia na vikosi vya usalama.
Vurugu hizo zilitokana na wafuasi wa chama cha kiislamu cha Muslim Brotherhood kushinikiza utawala wa kijeshi kumerejesha madarakani kiongozi wao aliyechaguliwa kidemokraia Mohamed Morsi.
Serikali imeongeza kuwa hata muda wa miezi miwili ukikamilika na hali ya usalama ikawa bado haijaimarika watalazimika kuongeza muda zaidi mpaka pale hali ya utulivu itakaposhuhudiwa nchi nzima.
Serikali ya Marekani hapo jana imeiandikia barua Serikali ya mpito ya Misri wakiitaka kuondoa hali ya hatari iliyowekwa mwezi mmoja uliopita ombi ambalo hata hivyo linaonekana kutofua dafu.
Jeshi nchini humo limekuwa likiendeleza operesheni za kuwakamata viongozi wa juu wa chama cha kiislamu cha Muslim Brotherhood ambapo mapaka sasa linamshikilia Mohamed Morsi na wafuasi wengine wa chama hicho zaidi ya elfu mbili.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi