. |
Leo ni Ijumaa tarehe 7 Dhilqaadi 1434 Hijria sawa na tarehe 13 Septemba 2013.
Siku kama ya leo miaka 763
iliyopita kulianza vita vya Mansuriya katika silsila ya Vita vya Msalaba
kati ya Wakristo na Waislamu. Vita hivyo vya kihistoria vilianzia
katika eneo lililofahamika kwa jina hilo huko Misri kati ya Saint Louis
mfalme wa Ufaransa ambaye alikuwa na lengo la kuitwaa Misri. Katika vita
vya Mansuriya Jeshi la Msalaba lilipigwa vibaya na wapiganaji wa
Kiislamu wa Misri waliokuwa wakiongozwa na Sallahuddin Ayubi. Na
hatimaye Saint Louis akakamatwa mateka na Waislamu na kufungwa jela
katika ikulu ya Loken ambayo hii leo inatumika kama jumba la makumbusho.
Miaka 233 iliyopita katika
siku kama hii ya leo lifti au elevator kwa kimombo ilivumbuliwa.
Mvumbuzi wa lifti hiyo ya kwanza alikuwa raia wa Marekani kwa jina la
John Bikbart. Lifti hiyo ilifanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza katika
mji wa Chicago nchini Marekani. Katika majaribio hayo, watu kadhaa
waliingia ndani ya lifti hiyo na kwenda juu na chini. Lifti ya kwanza ya
umeme ilitengenezwa mwaka 1889 na ile ya otomatiki mwaka 1915.
Na siku kama hii ya leo
mwafaka na tarehe 13 Septemba 1993 Yasir Arafat kiongozi wa zamani wa
Harakati ya Ukombozi wa Palestina PLO na Yitzhak Rabin waziri mkuu wa
wakati huo wa utawala haramu wa Israel walisaini mkataba wa mapatano kwa
jina la "Makubaliano ya Ghaza-Jericho" huko Washington, Marekani.
Harakati ya Ukombozi wa Palestina PLO na utawala wa Kizayuni
zilitambuana rasmi katika makubaliano hayo yaliyosainiwa miaka miwili
baada ya kuanza mazungumzo eti ya amani kati ya Waarabu na utawala wa
Kizayuni.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!