. |
Robert ‘Bobby’ Tufts hajaanza hata shule ya Nursery
ambayo huku Tanzania tunaifahamu kama chekechea au vidudu lakini tayari
ameshajiwekea historia ya kuwa mwanasiasa mwenye umri mdogo kuliko wote
duniani .
Dogo
huyo ameweza kuwa meya wa mji mmoja huko Minesotta akiwa na umri wa
miaka mitatu pekee, unaambiwa ni Meya wa mji mdogo wa Dorset ulioko huko
Minesotta Marekani na hii ni mara yake ya pili kuchaguliwa kuwa meya wa
mji huo baada ya kupigiwa kura siku ya jumapili ambapo aliweza kushinda
kipindi chake cha pili cha uongozi .
Mstahiki Meya wa Mji wa Dorset Robert ‘Bobby’ Tufts. |
Mji
huo una serikali ndogo inayoongozwa na meya huyo mdogo ambaye anaongoza
idadi ya watu 220 ambao ni wakazi wa mji huo ambapo kama ilivyo kwenye
manispaa yoyote, meya Bobby anaongoza serikali ambapo hufanya maamuzi
yanayohusu bajeti ya matumizi ya mji wa Dorsett pamoja na masuala
mengine nyeti kama ya kodi na makusanyo mengine ya mapato.
Mama
mzazi wa Meya Robert Tufts, Emma Tufts anasema kuwa moja ya agenda za
uongozi wa mwanaye ni kukusanya fedha kwa ajili ya taasisi ya misaada ya
Ronald McDonald iliyoko Dorset eneo la Red River Valley Fargo Dakota ya
Kaskazini pamoja na ujenzi wa kibao kipya cha kuwakaribisha wageni huko
Dorset kwenye barabara zinazopakana na miji mingine.
. |
Taarifa
za Meya huyo mdogo kuliko wote duniani zimefika mpaka ikulu kwa Barack
Obama ambae amempa Robert Tufts mwaliko maalum kwenye ikulu yake na ana
mpango wa kumfanya kuwa mshauri wake maalum kwenye mfuko wake
unaofahamika kama ObamaCare Foundation.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!