KIUNGO mahiri wa
kimataifa kutoka Ghana, Kevin Prince-Boateng amesisitiza kuwa Italia sio
nchi ya kibaguzi pamoja na uhamisho wake kutoka AC Milan kwenda Schalke
ya Ujerumani kuhusishwa na masuala hayo. Mapema
mwezi huu bwana fedha wa klabu ya AC Milan, Peter Peters alikaririwa
akidai kuwa uhamisho wa kiungo huyo ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na
matukio ya kibaguzi yaliyokuwa yakimuandama mara kwa mara akiwa
uwanjani. Lakini Boateng alikanusha tetesi hizo na kudai kuwa hakuondoka Milan kwa ajili ya matukio ya kibaguzi. Boateng
amesema hakuondoka Italia kwa ajili ya wahuni wachache ambao wamekuwa
wakiongoza vitendo vya kibaguzi na anaamini nchi hiyo sio ya kibaguzi
kama watu wanavyofikiria. Mchezaji
huyo amecheza Milan kwa misimu mitatu na kushinda taji moja la Serie A
kabla ya kurejea nchini Ujerumani katika kipindi cha usajili wa majira
ya kiangazi msimu huu.
Home »
michezo ulaya
» ITALIA SIO NCHI YA KIBAGUZI - BOATENG.
ITALIA SIO NCHI YA KIBAGUZI - BOATENG.
Written By Unknown on Thursday, 12 September 2013 | Thursday, September 12, 2013
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!