TIMU ya taifa ya Mexico
inaweza kushindwa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwakani kwa mara ya
kwanza baada ya kupita miaka 25 kama wakishindwa kushinda mechi zao
mbili ambazo ndio zitaamua hatma yao. Hali
imekuwa mbaya mpaka kufikia Shirikisho la Soka la Mexico kufikiria
uwezekano wa kubadilisha kocha wa timu ya taifa ambaye anatakuwa watatu
katika kipindi cha siku nne. Mbali
na hivyo pia vyombo vya habari vimeonyesha mapenzi madogo kwa wachezaji
baada ya kupoteza mchezo dhidi ya mahasimu wao Marekani kwa kufungwa
mabao 2-0 huko jijini Columbus, Ohio Jumanne. Kupoteza
mchezo dhidi ya Marekani kumekuja siku chache baada ya kupoteza mchezo
mwingine dhidi ya Honduras Ijumaa iliyopita hivyo kupelekea Mexico
kutupwa mpaka nafasi ya tano katika timu sita za kundi la CONCACAF. Katika
kundi hilo timu tatu za juu ndio zitafuzu moja kwa moja kwenda Brazil
huku timu ya nne itapelekwa kucheza hatua ya mtoano na New Zealand huku
mpaka sasa zikiwa zimebaki nafasi mbili pekee baada ya Marekani na Costa
Rica kufuzu kwa kuchukua nafasi mbili za juu.
Home »
michezo ulaya
» MEXICO HATIHATI KUFUZU KOMBE LA DUNIA.
MEXICO HATIHATI KUFUZU KOMBE LA DUNIA.
Written By Unknown on Thursday, 12 September 2013 | Thursday, September 12, 2013
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!