MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura 'Lady
Jaydee' a.k.a Annaconda, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kiatu
kirefu alichokivaa, kutaka kumwangusha jukwaani alipokuwa anatumbuiza
kwenye tamasha la hitimisho la Kili Music Tour.
Tukio hilo la kutaka kuanguka lilitokea mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni lilipofanyika tamasha hilo huku kiatu hicho kuonekana ndiyo chanzo cha msanii huyo kutaka kuanguka.
Msanii huyo alipanda jukwaani hapo akiwa amevaa 'High heels' kama
kawaida ya shoo zake, lakini siku hiyo kiatu hicho kilionekana kutaka
kumuumbua.
Jaydee alifafanua sababu ya kutokea kwa tukio hilo kwa kupitia ukurasa wake wa Twitter pamoja na Facebook, ambapo aliweka wazi kuwa kuanguka ni ajali kama ajali nyingine.
Msanii huyo ni miongoni mwa wasanii wenye mafanikio makubwa, huku akiwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike wachache wenye mafanikio ya kimuziki, ambapo anatamba na kibao chake cha Yahaya kilichomo ndani ya albamu yake ya 13.
Tukio hilo la kutaka kuanguka lilitokea mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni lilipofanyika tamasha hilo huku kiatu hicho kuonekana ndiyo chanzo cha msanii huyo kutaka kuanguka.
. |
Jaydee alifafanua sababu ya kutokea kwa tukio hilo kwa kupitia ukurasa wake wa Twitter pamoja na Facebook, ambapo aliweka wazi kuwa kuanguka ni ajali kama ajali nyingine.
Msanii huyo ni miongoni mwa wasanii wenye mafanikio makubwa, huku akiwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike wachache wenye mafanikio ya kimuziki, ambapo anatamba na kibao chake cha Yahaya kilichomo ndani ya albamu yake ya 13.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!