Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Ruto arejea tena Hague kuendelea na kesi yake

Ruto arejea tena Hague kuendelea na kesi yake

Written By Unknown on Tuesday, 17 September 2013 | Tuesday, September 17, 2013

William Ruto
Naibu Rais William Ruto akiwa kortini ICC
NAIBU Rais William Ruto aliondoka nchini KENYA kuelekea Hague Jumatatu huku kesi yake ikitarajiwa kuendelea tena katika mahakama ya ICC.
Huku akiandamana na mkewe, Rachel, Bw Ruto aliondoka kwa ndege ya shirika la Kenya Airways iliyoondoka kuelekea Uholanzi kutoka uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa mbili na nusu asubuhi.
Pamoja  na mtangazaji Joshua arap Sang, Bw Ruto anakabiliwa na mashtaka dhidi ya uhalifu wa kibinadamu katika mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kutokana na ghasia za 2008 zilizopelekea vifo vya zaidi ya watu 1,000 huku wengine 650,000 wakiachwa bila makao.
Maafisa wengine wakuu serikalini, wakiwemo wanasiasa na marafiki wake waliandamana naye katika uwanja huo kumuaga. Baadhi yao walikuwa Kiongozi wa Walio wengi Bungeni Aden Duale na mwenzake wa Seneti Kithure Kindiki.
Wengine walikuwa Maseneta Kipchumba Murkomen, Charles Keter, Lenny Kivuti, Paul Wamatangi, mawaziri James Macharia, Kazungu Kambi miongoni mwa wengine.
Mamake
Bw Ruto vile vile alisindikizwa na mamake Sarah. Taifa Leo ilifahamu Jumatatu kuwa wabunge wapatao 25 waliondoka nchini mnamo Jumapili jioni kuelekea Hague ili kuwapa motisha wawili hao.
Kabla ya kuondoka, Bw Ruto, ambaye alikuwa amevalia kofia yake kama kawaida, alitumbuizwa na waimbaji wa kundi la Nyakinyua.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi