Gavana wa Nairobi Dkt Evans Kidero. |
Wachuuzi hao
walidai kuwa ukatili huo umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu, na hawakuwa
na jingine ila kuelezea changamoto zao kwa njia ya maandamano.
Wachuuzi hao walikuwa wamepanga kuandamana kutoka mzunguko wa Globe na waelekee hadi Afisi ya Rais.
Kulingana na
mmoja wa viongozi wao Bw Kim Waweru, maandamanao hayo yalichochewa na
kisa cha hivi juzi, ambapo kijana mmoja aliyetambuliwa kama Mark Kyalo,
alipigwa risasi na kuuawa na polisi kwa madai ya kuhusika katika wizi.
Huku wakiwa
wamebeba mabango ya kukashifu dhuluma hizo, wachuuzi hao walionekana
kukaidi juhudi za mkuu wa polisi wa Nairobi ya Kati Bw Patrick Oduma,
aliyejaribu kuwahakikishia kuwa malalamishi yao yatachunguzwa na
kutekelezwa.
“Tunamuomba
yeyote aliye na habari kuhusu tukio hilo kujitokeza na kuandikisha
taarifa katika kituo cha polisi,” Bw Oduma akawarai waandamanaji hao
waliojawa na ghadhabu.
Gavana
Aidha,
aliwaomba wachuuzi hao kuwachagua viongozi wawakilishi wawili ambao
wangekutana na gavana wa Nairobi Dkt Kidero katika mkutano maalum wa
kuangazia changamoto zao.
Hata hivyo,
walikaidi agizo la mkuu huyo wa polisi kwa sharti kuwa hawangeshiriki
katika mkutano huo ikiwa waliohusika katika mauaji hayo hawajakabiliwa
kisheria.
Makabiliano
hayo yalipelekea msongamano wa magari katika barabara ya Monrovia.
Hakuna aliyeripitiwa kujeruhiwa katika makabiliano hayo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!