Takribani wajumbe waandamizi 50 kutoka Afrika, Ulaya na Ghuba ya Uarabuni walihudhuria mkutano wa siku moja huko Brussels, pamoja na vikundi vya misaada na taasisi za fedha duniani.
Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso (kulia) akimsalimia Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud kwenye makao makuu ya EU huko Brussels Jumatatu (tarehe 16 Septemba). |
Somalia ilipata tena “hadhi yake kama mwanachama mwenye uhuru kamili wa jumuiya ya kimataifa”, Barrosso alisema, akiongezea kwamba mengi yanahitajika kufanywa, akionyesha matatizo ya kiusalama na haki za binadamu.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alisema alikuwa na “shukrani nyingi” kwa jitihada zote zinazofanywa kwa niaba ya nchi yake, akibainisha vipaumbele vinne miongoni mwa kazi nyingi zilizo mbele yao -- usalama, mageuzi ya kisheria, ugharimiaji wa umma na ufufuaji wa uchumi.
“Somalia imepewa fursa kubwa ili isonge mbele,’’ alisema.
Hata hivyo, wanamgambo wa al-Shabaab walipuuza mkutano huo kama wa kupoteza muda.
“Mikutano kamwe haijawahi kuwa na matokeo yenye maana kwa mazingira yaliyopo hapa Somalia na huu hautakuwa tofauti. Ni kupoteza nguvu,” al-Shabaab walisema kupitia Twitter. “Mabilioni yaliyoahidiwa yana uwezekano mkubwa yasitolewe , sehemu ya kiasi kitakachotolewa kwa waasi wa dini itapotea katika rushwa na tutarudi palepale tulipokuwa.”
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!