KOCHA Manuel Pellegrini jana alikuwa
mwenye furaha baada ya timu yake, Manchester City kuanza vyema Ligi ya
Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya wenyeji Viktoria Plzen katika kundi lao D lenye timu za Bayern Munich na CSKA Moscow.
Dakika
10 zilitosha kwa City kutengeneza ushindi mnono na sasa wanaelekea
kwenye mchezo na mahasimu, Man United Jumapili wakiwa wenye kujiamini.
Edin
Dzeko alifunga la kwanza dakika ya 48, Yaya Toure akafunga la pili
dakika ya 53 na Sergio 'Kun' Aguero akakamilisha kazi dakika ya 58 kwa
bao la tatu.
kikosi
cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov,
Toure (Javi Garcia 80), Fernandinho, Jesus Navas/Milner dk67, Aguero,
Nasri, Dzeko/Negredo dk83.
Plzen:
Kozacik, Rajtoral, Hejda/Hubnik dk66, Prochazka, Limbersky, Horava,
Horvath, Petrzela, Kolar/Duris dk61, Kovarik, Bakos/Tecl dk84.
Salamu United: Wachezaji wa Manchester City wakishangilia ushindi wao wa ugenini dhidi ya Viktoria Plzen |
Mwanzo mzuri: Wachezaji wa Manchester City wakisherehekea kuanza vyema Ligi ya Mabingwa |
La kwanza: Edin Dzeko aliifungia bao la kwanza Manchester City |
Dzeko akishangilia baada ya kufunga |
Huwezi kuzuia mchomo huu: Kipa wa Viktoria Plzen, Matus Kozacik akirukia mpira uliopigwa na kiungo wa Manchester City, Yaya Toure (hayupo pichani) bila mafanikio, unapita kutinga nyavuni |
Yaya Toure akishangilia baada ya kufunga bao zuri kutoka nje ya boksi |
Samir Nasri akimtoka mchezaji wa Viktoria Plzen, Lukas Hejda |
Vitani: Sergio Aguero akipambana na Lukas Hejda |
. |
Aguero akishangilia baada ya kufunga bao la tatu |
Aguero akishangilia na Dzeko, na Toure na Nasri |
. |
Mwanzo mzuri: Manuel Pellegrini alifurahia ushindi wa ugenini jana |
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!