NYOTA
Gareth Bale ametokea benchi na kupikia mabao mawili Real Madrid
ikiitandika Galatasaray mjini Istanbul mabao 6-1 huku Cristiano Ronaldo
akipiga hat-trick yake ya 21 Bernabeu.
Bale aliwashuhudia Isco, Karim Benzema
na Ronaldo wakiiweka klabu yake mbele kwa mabao 3-0 kabla ya kuingia na
kutoa mchango wake kunenepesha ushindi.
Kwanza,
ilikuwa mpira wa adhabu wa winga huyo wa Wales uliomkuta Ronaldo,
ambaye akaifungia bao la nne timu ya Carlo Ancelotti. Kisha akampa pasi
Ronaldo, ambaye alimpasia pia Benzema kabla ya mshambuliaji huyo wa
Ufaransa kufunga bao lake la pili katika mchezo huo.
Isco
alifunga dakika ya 33, Benzema 54 na 81 Ronaldo 63, 66 na 90, wakati
bao la kufutia machozi la wenyeji lilifungwa na Bulut dakika ya 84.
Didier Drogba alicheza kwa dakika 45 tu kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Amrabat.
Kikosi
cha Real Madrid kilikuwa: Casillas/Lopez dk14, Carvajal, Ramos, Pepe,
Arbeloa, Modric/Illarramendi dk72, Khedira, Di Maria, Isco/Bale dk64,
Ronaldo na Benzema
Galatasaray: Muslera, Eboue, Chedjou, Nounkeu, Riera, Inan, Melo, Baytar/Bruma dk62, Yilmaz, Sneijder na Drogba/Amrabat dk46.
|
Anaondoka na mpira wake: Cristiano Ronaldo akiwa ameweka mpira kwenye jezi yake baada ya kufunga Hat-trick mjini Istanbul |
Katika
mechi nyingine, Man Utd imeshinda 4 -2 dhidi ya Bayer Leverkusen, Real
Sociedad imefungwa nyumbani 2-0 na Shakhtar Donetsk, FC Copenhagen
imetoa 1 - 1 na Juventus, Benfica imeifunga 2 - 0 Anderlecht,
Olympiacos imefungwa 4-1 nyumbani na PSG, Bayern Munich imeichapa 3 - 0 CSKA Moscow wakati Plzen imefungwa 3-0 nyumbani na Man City.
|
17 September |
|
|
Man Utd | 4 - 2 | Bayer Leverkusen |
Wayne Rooney (21)
Robin van Persie (58)
Wayne Rooney (69)
Antonio Valencia (78) |
| Simon Rolfes (53)
Omer Toprak (87) |
|
Old Trafford |
|
Report |
|
17 September |
|
|
Real Sociedad | 0 - 2 | Shakhtar Donetsk |
|
| Santos Alex Teixeira (64)
Santos Alex Teixeira (86) |
|
Anoeta |
|
Report |
|
|
17 September |
|
|
FC Copenhagen | 1 - 1 | Juventus |
Nicolai Jorgensen (13) |
| Fabio Quagliarella (53) |
|
Parken |
|
Report |
|
17 September |
|
|
Galatasaray | 1 - 6 | Real Madrid |
Umut Bulut (83) |
| Alarcon Isco (32)
Karim Benzema (53)
Cristiano Ronaldo (62)
Cristiano Ronaldo (65)
Karim Benzema (80)
Cristiano Ronaldo (90) |
|
Turk Telekom Arena |
|
Report |
|
|
17 September |
|
|
Olympiacos | 1 - 4 | PSG |
Vladimir Weiss (24) |
| Edinson Cavani (19)
Santos Thiago Motta (67)
Santos Thiago Motta (72)
Aoas Correa Marquinhos (85) |
|
Karaiskakis Stadium |
|
Report |
|
17 September |
|
|
Benfica | 2 - 0 | Anderlecht |
Filip Djuricic (3)
Anderson Luisao (29) |
|
|
|
Estadio da Luz |
|
Report |
|
|
17 September |
|
|
Bayern Munich | 3 - 0 | CSKA Moscow |
David Alaba (2)
Mario Mandzukic (40)
Arjen Robben (67) |
|
|
|
Allianz Arena |
|
Report |
|
17 September |
|
|
Plzen | 0 - 3 | Man City |
|
| Edin Dzeko (47)
Yaya Toure (52)
Sergio Aguero (57) |
|
Struncovy Sady |
|
Report |
|
|
Kazi nzuri: Cristiano Ronaldo akikumbatiana na Gareth Bale baada ya kufunga bao lake la pili |
|
Mchezaji ghali duniani...anatokea benchi: Bale aliingia kipindi cha pili kuisaidia Real Madrid kuisambaratisha Galatasaray |
|
Wawili ghali: Gareth Bale (kulia) akiongozana na Cristiano Ronaldo wakati akishangilia bao lake la pili |
|
ameenda hewani: Cristiano Ronaldo akishangilia bao lake la kwanza |
|
Kazi nzuri: Karim Benzema akishangilia bao lake |
|
Kimya kimya: Isco alifunga bao la kwanza |
|
Hasira: Cristiano Ronaldo akimlalamikia refa baada ya kuangushwa |
|
Benchi: Gareth Bale akiangalia mechi kutokea benchi kipindi cha kwanza kabla ya kuingia na kufanya kazi nzuri |
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!