Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » MPYA! Je nikueleze kitu? Hekaya za Kiafrika kwa utamaduni wa amani

MPYA! Je nikueleze kitu? Hekaya za Kiafrika kwa utamaduni wa amani

Written By Unknown on Thursday, 12 September 2013 | Thursday, September 12, 2013

Ni za kustaajabisha, sumbufu, kusisimua, cheshi au za kuhuzunisha. Hekaya huwavutia watu wa marika yote. Hadithi kumi zilizochaguliwa sio tu za kuburudisha, lakini pia zina maadili muhimu, ufahamu na hekima za mababu.
Barani Afrika, utamaduni wa kusimulia hadithi bado ni muhimu. Ni njia ya maridhiano isiyo na gharama na ya kudumisha utamaduni.
Wengi wetu tunakumbuka nyakati ambazo wazazi au mababu na mabibi zetu walipokuwa wakitusimulia hadithi za kufurahisha zilizotokea zamani. Ndiaye Ibrahima kutoka Senegal ni miongoni mwa waliohadithiwa. Hekaya kumi anazotusimulia katika mfululizo wa vipindi hivi vya Noa Bongo Jenga Maisha yako alihadithiwa na bibi yake na zina funzo la kuishi pamoja kwa maelewano na amani.
Wanyama wana nafasi muhimu katika hekaya hizi - warefu na wadogo, wenye nguvu na dhaifu, walio shujaa na waoga. Jiunge na simba, fisi, ngiri, tembo, nyoka na wengine wengi katika visa vyao. Mbali na kutuacha katika hali ya kutopata msisimko, hali wanazokabiliananazo na mizozo wanayolazimika kuitatua, yanaonekana kuwa mambo yanayofahamika kwa wengi wetu.
Sikiliza na ufurahie, kwani kuna msemo usemao: "Ndiyo hekaya yetu inakwenda baharini, na atakayekuwa wa kwanza kunusa marashi yake, ataingia peponi."
Vipindi vya Learning by Ear - Noa Bongo Jenga Maisha yako vinapatikana katika lugha sita: Kingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharic. Vinafadhiliwa na wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi