Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » MWANAUME NA MWANAMKE WALIOBADILI JINSIA WAAMUA KUWA WAPENZI....

MWANAUME NA MWANAMKE WALIOBADILI JINSIA WAAMUA KUWA WAPENZI....

Written By Unknown on Monday, 16 September 2013 | Monday, September 16, 2013


Nchini Marekani, yenye watu waliojibadili jinsia, 'transgender' wapatao laki tisa, vijana wawili kati yao wamependana kimapenzi na huenda wakaoana.

Kijana Arin Andrews alizaliwa katika jinsia ya kiume, wakati binti Katie Hill alizaliwa katika jinsia ya kike.

Hivi karibuni, Arin alifanyiwa upasuaji wa kuondoa matiti yake (mastectomy) na kuanza kutumia vichocheo
Picture
Arin Andrews (kulia) na mwandani wake Katie Hill

vya hormone za kiume (testosterone) ili kujenga umbo la kiume kama anavyoonekana kulia kwenye picha. Alipoulizwa ikiwa hakujali kuwa na makovu kifuani mwake kwa ajili ya kuondoa matiti, alisema alikuwa radhi aishi na makovu kuliko kubeba matiti.

Akizungumza na wanahabari wa INSIDE EDITION, Arin ambaye awali alitambulika kwa jina la Emerald, anasema asingeweza kufikia hapo ikiwa asingepata upendo na ushirikiano kutoka kwa mpenziwe, Katie ambaye anayeelewa fika yanayoendelea kwenye kichwa chake.

Katie ambaye awali alitambulika kwa jina la Lucas, sasa hunyoa miguu yake ili isiwe na vinyweleo vingi kama mwanaume, jambo ambalo anasema lilimkosesha raha kila mara alipojitizama kwenye kioo kwa kujiona mbaya na asiyevutia. Anasema siku moja alipochoshwa sana na mawazo, alisema leo ni leo, liwalo na liwe; Akamketisha kitako mama yake na kumwambia "Usiku wa leo nitajiua endapo hutanisaidia," na hapo ndiyo ukawa mwanzo wa kuanza taratibu za kufanyiwa upasuaji wa kujibadili jinsia.

Mwaka jana, wazazi wa watoto hao wawili waliwakutanisha, na hapo ndipo mapenzi baina yao yalipowaka.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi