Kundi la vijana wenye mafungamano na wanamgambo wa Kituareg nchini Mali,
limezuia kutua ndege iliyokuwa imewabeba mawaziri watatu wa serikali ya
Mali, katika uwanja wa ndege wa mji wa Kidal kaskazini mashariki mwa
nchi hiyo. Mawaziri hao wa usalama, mipango na maridhiano ya kitaifa,
walikuwa wamefanya safari mjini Kidal kwa minajili ya kufanya mazungumzo
na wanamgambo hao wa Kituareg, lakini walijikuta katika hali ngumu
baada ya kundi kubwa la vijana wa kabila hilo kuishambulia kwa mawe
ndege yao wakati wa kutua. Kwa mujibu wa ripoti hiyo tume ya uthabiti ya
Umoja wa mataifa nchini Mali kwa kusaidiwa na serikali, iliweza kufanya
maelewano na hivyo kufanikisha ndege hiyo kutua uwanjani hapo kwa
usalama. Aidha ripoti hiyo inaelezea kutupwa maguruneti mawili katikati
ya mji huo bila
Home »
siasa afrika
» Watuareg wazuia ndege ya mawaziri kutua mjini Kidal
Watuareg wazuia ndege ya mawaziri kutua mjini Kidal
Written By Unknown on Monday, 16 September 2013 | Monday, September 16, 2013
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!