Roberto
Carlos amewaonya Chelsea kwamba mshambuliaji wao mpya Samuel Eto'o
anaweza kawa na ushawishi mbaya ndani ya chumba cha kubadilishia nguo.
Mkurugenzi
huyo wa zamani wa timu ya Anzhi Makhachkala amesema kwamba mshambuliaji
huyo mcameroon aliingilia majukumu yake ya kazi wakiwa pamoja katika
klabu hiyo ya Russia mpaka kufikia hatua kwamba alianza kufikiria
kujiuzulu.
Mwaka
2011, Carlos alikuwa Anzhi wakati timu hiyo ilipomnunua Eto'o kutoka
Inter Milan, na kumfanya mchezaji huyo kuwa mwanasoka anayelipwa fedha
nyingi zaidi duniani.
Baada
ya kufunga mabao 36 katika mechi 71 akiwa na Anzhi, Eto'o amehamia
Chelsea kwa uhamisho huru na anaweza kuanza katika mechi yake ya kwanza
dhidi ya Everton jumamosi hii.
Lakini mahojiano na gazeti la Globo, Carlos ameelezea na namna Eto'o alivyomfanyia wakati wakiwa Anzhi.
Alisema: 'Nimemfahamu Eto'o tangu nikiwa na miaka 16, na kutokea wakati huo amekuwa mtu mzuri kwangu niliyempenda.
'Ni mtu mzuri, lakini kuna kitu kuhusu yeye 'ubinafsi' ndio kinachoharibu sifa yake.
'Wakati
mchezaji ambaye badala ya kucheza vizuri - hukaa na kujariu kulazimisha
kusajiliwa kwa wachezaji ambao ni marafiki zake - ni suala la
kusikitisha na linachanganya na kushangaza hasa kwa mchezaji kama Eto'o.
Alifanya yote haya akiwa Anzhi lakini sio kucheza soka la kiwango
kikubwa.'
Akizungumiza
namna mahusiano yao yalivyoharibika, Carlos alisema: 'Nilienda kwenye
klabu na katika mwaka wangu wa kwanza timu ilimaliza kwenye nafasi tano
za juu.
'Tuliweza
kuiweka timu kuwa katika ueledi wa 100%. Mwaka wa pili, tukamsaini
Eto'o na nilikuwa na control ya timu - Nilifanya kazi na wachezaji na
makocha. Nilifanya kazi nzuri katika kuifanya Anzhi kuwa miongoni mwa
timu bora.
'Kuwasili
kwa Eto'o, huku thamani ya kila ikijulikana, nilipata matatizo kidogo
katika chumba cha kubadilishia nguo na ikabidi niongee na wachezaji wa
kirusi na kuwaelezea kwanini Eto'o alikuwa pale.
'Japokuwa,
ukafika wakati Eto'o akaanza kuingilia majukumu yangu, kutaka kuwa na
mamlaka ndani ya timu, majukumu yangu na yale ya kocha Guus [Hiddink].
'Tuliongea
kuhusu jambo moja, na baada hapo alikuwa anaenda kwa wachezaji
anawaambia jambo lingine. Hilo lilinikera sana na nilionya ningeondoka.
'Hakuna aliyeniamini kwa sababu nilikuwa na mkataba wa miaka minne. Lakini baadae niliwaita Anzhi na kufikia makubaliano.'
Carlos,
40, tangu wakati akaondoka na sasa anafanya kazi kama mkurugenzi wa
timu Sivasspor huko Turkey. Mmiliki wa Anzhi Suleyman Kerimov aliamua
kuondokana na matumizi makubwa ya klabu na kupelekea kuuzwa kwa
wachezaji kadhaa.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!