Vikosi vya usalama vya Somalia vimezuia zaidi ya mashamulizi 200 ya al-Shabaab mjini Mogadishu katika mwezi wa Agosti kwa msaada wa kitengo kipya ya askari kanzu, Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa Abdikarim Hussein Guled salisema siku ya Jumamosi (tarehe 14 Septemba).
"Tumeanzisha kitengo cha askari kanzu kilichopelekwa ndani ya sekta nyingi za umma ili kukusanya habari za kuaminika na yeyote anayetishia usalama," Guled aliiambia Redio Mogadishu inayoendeshwa na serikali. Alisema kuwa kitengo hicho kipya kilianza kazi mwezi Julai.
Katika mwezi wa Agosti pekee, polisi walipokea fununu 330, alisema, ambapo asilimia 65 zilikuwa habari za kuaminika kuhusu mashambulizi ya ghafla ambayo yalijumuisha majaribio ya mauaji na ulipuaji mabomu ambayo mamlaka husika ziliweza kuyazuia.
Waziri aliapa kuwa serikali itaendelea kuendesha operesheni za usalama ili kuimarisha hali ya usalama ya Somalia na kuhakikisha usalama wa umma.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!