Jeshi la nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo limeshutumu
vikosi vya Rwanda kuvuka mpaka siku ya Jumapili na kumteka nyara mmoja
wa maafisa wake wa kijeshi, mashariki mwa nchi hiyo. Duru za Kijeshi
zinasema kwamba Sargenti Mulanga Kusakala ambaye alikuwa ametembelea
familia yake na wakati akitembea katika eneo lisilo kuw ana mwenyewe
kwenye mpaka baina ya nchi hizo mbili ndipo askari polisi watatu wa
Rwanda walimteka na kumpeleka nchini Rwanda.
Msemaji wa Jeshi la Congo jimboni kivu ya kaskazini Olivier
Hamuli amesema tukio hilo ni la utekaji nyara kwa kuwa Mwanajeshi huyo
alikuwa kwenye ardhi ya nchi yake na si nchini Rwanda, na taarifa hiyo
ya kutekwa kwa mwanajeshi huyo ilitolewa na wananchi baada ya hali
kuonekana kuwa mbaya ambapo amsema wamelazimika kupunguza ghadhabu ya
wananchi waliokuwa na hasira ambao waliandamana kwenye mpaka baina ya
Rwanda na DRCongo.
Maandamano hayo yalisababisha mipaka yote kufungwa kwa muda kabla ya kufunguliwa tena baada ya ghadhabu ya wananchi kupungua ili kuruhusu watu kureja nyumbani kutoka kila upande.
kwa mujibu wa mashahidi kutoka Goma, hali bado ni tete katika eneo hilo la mpaka, kwani wananchi wengi walikuwa bado ni wengi katika eneo la mpaka ambapo baadae jioni wanajeshi wa DRCongo na polisi walimiminika kwa wingi katika eneo hilo.
Kulingana na msemaji wa jeshi la DRCongo FARDC, Olivier Hamuli, Sergenti Mulanga Kusakala ni mwenye asili ya Mkoa wa Bandundu magharibi mwa Congo na anatumikia katika kanda ya kumi ya kijeshi katika mji wa Bukavu, mki mkuu wa Mkoa wa Kivu ya Kusini.
Mamlaka ya Rwanda imesema kuwa wamemkamata mwanajeshi wa congo aliyekuwa na Silaha nzito katika ardhi yao wakati Wanajeshi wa Rwanda walipokuwa wakifanya doria mjini Rubavu mji unaotenganisha nchi hizo mbili.
Uhusiano kati ya Rwanda na DRCongo umekuwa mbovu tangu mwezi Mei 2012 wakati waasi wa kundi la M23 walipoanza uasi dhidi ya serikali na ambapo wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakizilaumu Rwanda na Uganda kuwaunga mkono waasi hao, jambo ambalo nchi hizo zimekuwa zikikanusha.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!