Rais wa Ufaransa Francois Hollande akimpokea mwenyeji wake Joh Kerry |
Rais wa Ufaransa Francois Hollande
akiambatana na waziri wake wa mambo ya nje Laurent Fabious,
wamewapokea mapema leo asubuhi, mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza
William Hague na John Kerry wa Marekani ambao wanajadili kuhusu
muswada wa rasimu ambao viongozi wanatarajia kupasisha kabla ya juma
hili kumalizika.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabious
amesema nchi yake itazingatia ripoti ya wakaguzi wa Umoja wa Mataifa
kuhusu mauaji ya Damascus inayotarajiwa kutolewa Jumatatu ili kusitisha
msimamo wake. Ameyasema hayo wakati alipompokea katika katika Ikulu ya
rais ya Quai d'Orsay mwenziye wa Uingereza, na kuungana na waziri wa
mambo ya nje wa Uturuki, Ahmet Davutoglu.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban
Ki-moon, ripoti hiyo ya wakaguzi kuhusu matumizi ya silaha za Kemili
itahitimisha matumizi ya silaha hizo bila kutaja muhusika wa mauaji ya
watu 21 Aout yaliosababisha mauaji ya watu elfu moja na mia tano, kwa
mujibu wa Marekani.
Kwa mujibu wa duru za kidiplomasia, serikali ya
Paris inapanga kutumia ripoti hiyo ili kupata uunfgwaji mkono kwenye
Umoja wa Mataifa, ambapo rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema
inabidi kuandaa vikwazo iwapo hakutakuwa utekelezwaji wa mkataba na
kwamba kuharibu silaha za kemikali ni hatuwa ya kwanza muhimu, lakini
sio njia ya kufikia suluhu ya mzozo wa kisiasa nchini Syria.
Ma waziri wa mambo ya nje wa Marekani Johna Kerry
na mwenziwe wa Urusi Sergei Lavrov wameafiki kukutana Septemba 28 ili
kupanga kalenda ya mkutano wa amani kuhusu Syria.
Urusi inaweza kuunga mkono uingiliaji kijeshi
nchini Syria iwapo serikali ya Syria itakiuka makubaliano. Hata hivyo
waziri Lavrov amesema Urusi itafanya uchunguzi kuhusu taarifa zote za
tuhuma dhidi ya serikali ya Syria.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!