Niko sawa: Kulikuwa kuna hofu kwamba maumivu aliyoyapata Olivier Giroud dhidi ya Sunderland yatamuweka nje |
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Olivier Giroud
amepunguza hofu juu ya majeruhi aliyoyapata katika mchezo wa Ligi Kuu ya
England dhidi ya Sunderland juzi.
Mshambuliaji huyo alitolewa nje mwishoni
mwa mchezo na Arsene Wenger akasema ana wasiwasi wa kumkosa mpachika
mabao huyo kikosini mwake.
Lakini Mfaransa huyo, ambaye amefunga
mabao katika kila mechi ya ligi hadi sasa, amesema atakuwa fiti
kuichezea The Gunners katika mchezo mkali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya
Jumatano dhidi ya Marseille.
Hofu imepungua: Arsene Wenger alikuwa ana wasiwasi wa kukosa washambuliaji Jumatano |
Santi Cazorla anatakiwa kuwa nje hadi
katikati ya Oktoba na alipoulizwa juu ya maumivu yake, Giroud alisema:
"Si mbaya hakika, si mbaya kama nilivyohofia awali. Nilipata pigo mapema
mchezoni, lakini hakuna aliyekuwa karibu yangu wakati naumia wakati
huo,"alisema.
"Nilikuwa nawania mpira nikadondokea mguu. Nikaumia kifundo cha mguu, lakini bahati nzuri, hakuna maumivu makubwa. Nipo vizuri, kweli nitakuwa safi (kwa mechi na Marseille),".
Giroud anatakiwa kutambua ukweli kwamba
alisajiliwa baada ya kuondoka kwa Robin van Persie Emirates msimu
uliopita, na kiwango chake kinaenda kikikua tangu msimu uliopita.
Ameanza vizuri msimu huu na kuna
matumaini atafanya vizuri zaidi hasa baada ya kusajiliwa kwa kiungo
Mjerumani, Mesut Ozil kwa dau la Pauni Milioni 42.5 kutoka Real Madrid.
Na moto: Giroud amefunga bao katika kila mechi ya Ligi Kuu England msimu huu |
. |
Mtaalamu wa pasi za mabao: Lakini
amesema kazi yake inakuwa rahisi zaidi kutokana na wachezaji kama Mesut
Ozil (kulia) kumpa pasi za mabao
"Huu ni mwendo mzuri ninaokwenda nao tangu nimejiunga na Arsenal na ninafikiri kinaweza kuwa kiwango kizuri zaidi.
Na sasa tuna mchezaji wetu mpya, itakuwa nzuri zaidi.
"Wote tulijua juu ya ubora wake (Ozil), lakini unapokuwa unacheza naye uwanjani ni nzuri sana.
"Wakati wote anatazama nafasi na
anafanya mambo haraka anapoona mwanya, ni rahisi sana. Unaweza kuona
mapema ataifanya hii timu kuwa bora. Lakini ngoja tuone, kwa ubora wake,
anaweza kufanya timu yoyote duniani iwe bora.
"Sasa kila mshambuliaji ana bahati ya
kutosha kuwa na wachezaji kama Ozil, Aaron (Ramsey), Jack (Wilshere),
Theo (Walcott) na (Santi) Cazorla nyuma yake. Nahisi bahati sana,".
Arsenal inakwenda Stade Veledrome
kumenyana na Marseille ikihitaji matokeo mazuri katika kundi lake ambalo
lina timu pia za Napoli na Dortmund.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!