wapiganaji waasi wa kundi la MNLA kaskazini mwa Mali |
Hata hivyo serikali ya Bamako haikulipa
uzito tukio hili na kulichukulia kama la kawaida ambapo jeshi la
serikali lilipamabana na majambazi wenye silaha katika opresheni yao ya
usalama wakati nchi hiyo ikielekea kujizatiti katika eneo la kaskazini
lililokuwa chini ya mikono ya waasi wa Tuareg na wale wa makundi ya
jihadi.
Uongozi wa kijeshi wa kundi hilo umetowa amri kwa
wapiganaji wote wa kundi hilo waliopo katika eneo la kaskazini kujibu
mashambulizi na kujihami kikamilifu iwapo watashambuliwa na kuhakikisha
wamewasambaratisha wanajeshi wa serikali ya Bamako.
Msemaji wa kundi la MNLA amelaani vikali
mashambulizi ya juma lililopita na kuyaita kuwa ni uvunjifu wa mkataba
wa kusitisha mapigano ambapo serikali ya Bamako imeshindwa kuheshimu na
kwamba hawatokubali ukatili unaofanyw a na wanajeshi wa Mali dhidi ya
raia wenye asili ya kitureg.
Mossa Ag Attaher amesema kuwa wanasubiri viongozi
wapya wa Mali kutowa muelekea ulio wazi na chanya kuhusu nia thabiti ya
kuendeleza majadiliano juu ya kufikia hatuwa za kisheria na kisiasa
kuhusu eneo la Azaward katika muda uliokubaliw akwenye mkataba wa amani
uliosainiwa mjini Ouagadoudgou.
Mbali na hivo amesema kundi hilo la MNLA
litachukuwa jukumu lake la kulinda maslahi ya wananchi wa eneo la
Azaward wakitumia njia zote.
Kundi la MNLA na lile la HCUA ambalo pua ni kundi
la waasi wa Tuareg walifikia kwenye mkataba wa amani na serikali ya
Bamako Juni 18 mjini Bamako, mkataba ambao uliruhusu kufanyika kwa
uchaguzi wa Julay 28 katika mji wa Kidal, kaskazini mwa Mali, ambao
ulikuwa chini ya udhibiti wa makundi ya kijeshi ya Touareg baada ya
operesheni ya vikosi vya Ufaransa vilivyo yafurusha makundi ya jihadi
yanayofungamana na kundi la kigaidi la Alqaida katika eneo la Maghreb la
Aqmi.
Mkataba huo, unaagiza usitishwaji mapigano,
kurejea hatuwa kwa hatuwa kwa wanajeshi wa Mali mjini Kidal na
kukusanywa katika eneo maalum kwa wapiganaji waasi.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!