MWENYEKITI wa klabu ya
Crystal Palace, Steve Parish ametaka wachezaji wanaojirusha kuonyeshwa
kadi nyekundu moja kwa moja badala ya kadi ya njano kama ilivyo hivi
sasa. Kauli ya
bosi huyo imekuja kufuatia Ashley Young wa Manchester United kupewa kadi
ya njano kwa kujirusha baada ya kugongana na Kagisho Dikgacoi wa Palace
katika mchezo baina ya timu hizo iliyochezwa Jumamosi. Dikgacoi
alitolewa baadae kwa kadi nyekundu baada ya kugongana tena na Young
katika mchezo huo ambao United waliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Parish
amesema kama beki akimzuia mshambuliaji aliyekuwa katika nafasi ya
kufunga anapewa kadi nyekundu ya moja kwa moja haoni sababu ya kwanini
wachezaji wanaojirusha ili kutengeneza nafasi za kufunga nao kupewa kadi
nyekundu pia. Katika
mchezo huo mwamuzi Jon Moss alimpa kadi ya njano Young kwa kujirusha
katika tukio la kwanza lakini baadae mwamuzi alitoa penati kwa wenyeji
kwa faulo aliyofanyiwa Young na Dikgacoi ambaye alipewa kadi nyekundu. Young
amekuwa akilalamikiwa hata na makocha wake kwa tabia yake ya kujirusha
ambapo kocha wa zamani wa United Sir Alex Ferguson aliwahi kusema kuwa
mchezaji huyo anaanguka kirahisi sana.
Home »
michezo ulaya
» WACHEZAJI WANAOJIRUSHA WANASTAHILI KUPEWA KADI NYEKUNDI YA MOJA KWA MOJA.
WACHEZAJI WANAOJIRUSHA WANASTAHILI KUPEWA KADI NYEKUNDI YA MOJA KWA MOJA.
Written By Unknown on Monday, 16 September 2013 | Monday, September 16, 2013
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!