Watu 11 wanaoshukiwa kuwa Wafuasi wa kundi la Wanamgambo wa
kiislamu wa Boko Haram wamekamatwa na makundi ya vijana waliojitolea
kupambana na Wanamgambo hao na kisha kuwakabidhi wanajeshi wa nchini
Nigeria, Kamanda wa Jeshi katika eneo hilo ameeleza na kuthibitisha
kuwa Watu wannne kati yao wamepoteza maisha wakiwa kizuizini.
Luteni Kanali Beyidi Martins amelipongeza
kundi hilo la vijana ambao wanaasili ya mji wa Maiduguri mji mkuu wa
jimbo la Borno jirani na Adamawa ngome ya Boko Haram wenye kujihami kwa
mapanga na marungu.
Vijana hao walitoka Maiduguri kuelekea Michika
wakiwafuata watuhumiwa hao wa ugaidi wa kundi la Boko Haram na
kufaanikiwa wakiwa pamoja na watu watano waliowapa hifadhi na
walitukabidhi, amesema kanali Beyidi Martins.
Washukiwa wanne walipoteza maisha siku ya Jumamosi
na Jumapili katika majengo ya jeshi kufuatia majeraha walioyapata
wakati wa kukamatwa kwao.
Jimbo la Borno ndiko kuliko ngome ya wapiganaji wa
kundi la Boko Haram ambapo limezidisha hujuma katika kipindi cha miezi
mitatu iliopita mashambulizi dhidi ya makundi ya vijana wanaojihami na
ambao wamekuwa wakipewa mafunzo na kupongezwa na jeshi.
Vinaja wa makundi hayo yakujihami wamefaulu
kuwafurusha wapiganaji wa Boko haram katika mji wa Maiduguri na
kuwapeleka hadi mpakani mwa Cameroon, Tchad na Niger.
wapiganaji wa kundi la Boko Haram
|
Kundi hilo la Boko Haram limekuwa likidai uundwa
wa taifa la kiislam kaskazini mwa Nigeria ambapo mapambano yamekwisha
dumu sasa miaka minne. Tangu mwanzoni mwa mwezi Mei, jeshi limekuwa
likiendesha operesheni katika maeneo yaliotangazwa hali ya hatari ili
kukomesha uasi huo.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la haki za
binadamu la Human Right Watch Machafuko ya kundi la Boko Haram
yamesababisha zaidi ya watu elfu tatu na mia sita kupoteza maisha tangu
mwaka 2009
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!