Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » AJALI KUBWA YATOKEA MJINI NAIROBI WATU ZAIDI YA 10 WARIPOTIWA KUFARIKI DUNIA

AJALI KUBWA YATOKEA MJINI NAIROBI WATU ZAIDI YA 10 WARIPOTIWA KUFARIKI DUNIA

Written By Unknown on Wednesday, 30 October 2013 | Wednesday, October 30, 2013

Ajali ya gari la Moshi nchini Kenya

Zaidi ya watu 10 wamepoteza maisha na wengine zaidi 30 kujeruhiwa nchini Kenya baada ya gari moshi kuligonga gari la abiria jijini Nairobi Jumatano asububi.

Kamanda wa polisi jijini Nairobi amethibitisha ajali hiyo na kueleza kuwa  ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo lililokuwa na abiria kujaribu kuvuka reli kabla ya gari la moshi kufika lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa.
Shirika la Msalaba mwekundu liliwasili katika eneo la ajali haraka na kuwakimbiza waliokuwajeruhiwa Hospitalini ili kuzuia idadi kubwa ya watu kupoteza maisha.
Polisi jijini Nairobi wanasema kuwa wamemshikilia dereva wa basi hilo kwa kile wanachosema kuwa ana makosa ya kuvuka reli wakati gari hilo la Moshi likiwa katika mwendo wa kasi.
Ajali nchini Kenya mara nyingi husababishwa na madereva hasa wa magari kutotii sheria za barabarani na kusababisha zaidi ya watu elfu tatu kupoteza maisha kila mwaka kwa mujibu wa takwimu za  polisi wa trafiki nchini humo.
Mwaka 1993 Kenya ilishuhudia ajali mbaya ya gari la Moshi wakati lilipoanguka mtoni likiwa njiani kwenda jijini Nairobi kutoka Mombasa na kusababisha vifo vya watu 140 wengine wao wakiwa watalii.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi