Msanii Bob Junior amefunguka Jana kupitia vyombo vya habari kuwa yuko single baada ya ndoa yake kuvunjika mwezi moja uliopita. Wasanii wengi huwa wanapata wakati mgumu wanapo funga ndo kwa sababu ya umaarufu na ratiba za maisha yao kabla ya kufunga ndoa.
Bob Junior jana mchana ametambulisha wimbo wake mpya na kutoa taarifa kwa mabinti wote kuwa kwa sasa Bob Junior ni single boy kumanisha kuwa ameachana na mke wake mwezi moja uliopita. Kuogopa kuweka mambo ya familia waze Bob Junior hajasema haswa Sababu ya kuachana na mke wake ila amesema kilicho changia ndoa yake kuvunjika ni Wivu wa mke wake.
Bob junior amesema kuwa wivu ni moja ya sababu zilizofanya ndoa yake kuvunjika na kwamba alikuwa na wakati mgumu sana kumuonyesha mke wake kuwa yeye ni muaminifu kutokana na kuwa star na kupendwa na mashabiki wa Kike.
Fahamu kuwa ndoa ya Bob Junior Imedumu kwa Mwaka Moja Na miezi 2 tu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!