Waziri wa Ulinzi wa Somalia, Abdihakim Haji Mohamud Fiqi alihudhuria bunge la Somalia siku ya Jumatano (tarehe 9 Oktoba) kwa kuhojiwa juu ya hali ya usalama nchini, iliripoti Redio RBC ya Somalia.
Kamati ndogo ya ulinzi ya bunge ilimuhoji Fiqi juu ya kulipa vifaa vipya Jeshi la Taifa la Somalia na operesheni za usalama zinazoendelea dhidi ya al-Shabaab.
"Tumeanzisha mfumo mpya ili kuanzisha sheria kali za jeshi huku pia tukimaliza usajili wa wanajeshi," alisema Fiqi. "Jeshi letu lilikomboa maeneo mapya hivi karibuni ikiwemo Mahaday na Burane kutoka kwa makundi ya kigaidi, na hivi karibuni tunaelekea kwenye mikoa mipya kuwapa amani raia wetu."
Hivi karibuni Fiqi alisema operesheni zitaanza hivi punde kuwaondoa al-Shabaab kwenye ngome yao ya mji wa pwani wa Barawe.
"Tunadhamiria na kupanga kuukomboa hivi karibuni," alisema Jumanne kwenye mahojiano na Idhaa ya Amerika. "Na kama unavyojua, kwa kweli, popote al-Shabaab tunapowashambulia, hawarudishi mashambulizi, hawajalindi, huhama tu na kukimbia."
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!