Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HALI USALAMA NCHINI SYRIA SI YAKURIZISHA MAPIGANO YAZIDI KUPAMBA MOTO

HALI USALAMA NCHINI SYRIA SI YAKURIZISHA MAPIGANO YAZIDI KUPAMBA MOTO

Written By Unknown on Thursday, 17 October 2013 | Thursday, October 17, 2013

Waasi wa jeshi huru nchini Syria wameendesha shambulio jana katika jela la mjini Aleppo lililo chini ya udhibiti wa wanajeshi ya serikali ya rais Bashar Al Assad kaskazini mwa taifa hilo. Machafuko yameshika kasi nchini humo tangu pale wataalamu wa kuharibu silaha za nyuklia ambao tayari wamechunguza vituo kumi na moja vya bomu za kemikali nchini humo.

Kulingana na shirika la haki za binadamu nchini humo, Jana jioni, mapambano makali yameshuhudiwa baina ya waasi wa upinzani na jeshi la serikali linalomiliki jela hiyo.
Jela hiyo ambao ni kubwa zaidi nchini humo na ambamo wanazuiliwa watu wengi, imekuwa ikishambuliwa tangu mwezi April na makundi ya waasi wanataka udhibiti.
Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali vimesema jeshi la serikali likiungwa mkono na vikosi vya kundi la Hezbollah na wapiganji kutoka nchini Iraq wamepiga hatuwa katika uwanja wa mapambano kwa kuuteka mji wa tatu wa Boueida, taarifa ambayo imethibitishwa na shirika linalo tetea haki za Binadamu nchini humo.
Katika eneo la kusini mwa nchi hiyo takriban watu 21, wakiwemo watoto 4 wamepoteza maisha katika shambulio la kujitowa muhanga mjini Deraa. Wanahrakati wameituhumu serikali kutega bomu barabarani, wakati kituo cha habari cha serikali Sana kikisema kwamba magaidi 21 waliuawa wakati walipokuwa wanatega bomu ndani ya gari.
Wakati mapigano hayo yakiendelea, shirika la kimataifa linalopiga vita silaha za kemikali ambalo linaendesha shughuli ya kukagua vituo vya silaha za kemikali nchini Syria, limetangaza kwamba, limemaliza ukaguzi wake katika vituo 11 vilivyo wasilishwa na serikali ya rais Bashar al Assad.
OIAC imesema pia kwamba imekaguwa shughuli za kuharibu vifaa vinavyotengeneza bomu hizo zenye sumu katika vituo sita.
Wakaguzi wa kimataifa zidi ya sitini wanaelekeza nguvu katika orodha ya vituo iliowasilishwa na serikali ya Syria Septemba 19 ambapo inadaiwa kuwa na vituo 20 vya kutengeneza na kuhifadhi silaha za Kemikali.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi