Rais wa
Rwanda, Paul Kagame amesema nchi yake haitishwi
na hatua iliyochukuliwa
na serikali ya Marekani kusitisha msaada wake wa kijeshi kwa nchi hiyo
kwa kile inachodai Rwanda inawafadhili waasi wa M23 wanaopigana na
serikali mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.
Rais Kagame amesema anashangazwa na hatua ya Marekani kuihukumu
nchi hiyo kwa makosa ambayo Rwanda haihusiki kwa lolote wala haifadhili
kundi lolote la waasi nchini DRC na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni
kutoitendea haki Rwanda.
Rais Kagame amesema kamwe Rwanda haijawahi kuhusisha watoto wadogo kwenye jeshi lake wala kuunga mkono kutumikishwa kwa watoto wadogo kama wanajeshi kwenye kundi la M23.
Serikali ya Marekani ilitangaza majuma kadhaa yaliopita kusitisha msaada wake wa kijeshi kwa serikali ya Rais Kagame kufuatia hatuwa hiyo inayotajwa ya kuwafadhili waasi wa kundi la M23 wanaopambana na serikali ya Rais Joseph Kabila.
Umoja wa Mataifa kupitia wataalamu wake, umekuwa ukitowa ripoti kuhusu msaada wa hali na mali unatotolewa na serikali ya Rwanda kwa waasi wa kundi hilo, huku wapiganaji ambao wamekuwa wakijisalimisha kwenye kikosi cha kulinda amani nchini DRCongo wamekuwa wakitowa ushuhuda kuhusu msaada huo.
Hivi karibuni wapigani kadhaa wa kundi hilo walitoroka na kudaikuwa walisajiliwa kujiunga katika kundi hilo kutokea nchini Rwanda.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!