Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HALI YA SINTOFAHAM YAZIDI KUZUKA BAADA YA MAKATAA YA AU KUHUSU ICC MWISHONI MWA JUMA

HALI YA SINTOFAHAM YAZIDI KUZUKA BAADA YA MAKATAA YA AU KUHUSU ICC MWISHONI MWA JUMA

Written By Unknown on Monday, 14 October 2013 | Monday, October 14, 2013

Kikao cha viongozi wa Umoja wa afrika AU
Hatua ya viongozi wa Umoja wa Afrika AU, kutoa makataa kwa mataifa ya magharibi na mahakama ya kimataifa ya ICC kuhusu kuahirishwa kesi dhidi ya viongozi wa Kenya imeendelea kuzua hali ya sintofahamu kwa jumuiya ya kimataifa.

Mwishoni mwa juma viongozi wa Umoja wa Afrika waliokutana mjini Addis Ababab, Ethiopia kwa kauli moja walikubaliana kuiandikia barua mahakama ya ICC na baraza la Umoja wa mataifa UN kutaka kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ziahirishwe mpake pale watakapomaliza muda wao wa uongozi.
Viongozi hao wamekubaliana kuwa Kuanzia sasa hakuna Kiongozi wa nchi yoyote ya Afrika atakayepelekwa ICC au Mahakama yoyote wakati akiwa madarakani,
Kiongozi yoyote yule ambaye Katiba inamruhusu kukaimu Urais naye hatapelekwa ICC akiwa madarakani, Viongozi wa Afrika wanaotuhumiwa makosa washtakiwe baada ya kumaliza mihula ya uongozi.
Viongozi wa Afrika wamesikitishwa na mwenendo wa ICC, toka 2004, kati ya kesi 30, kesi 27 ni kutoka nchi za Bara la Afrika, Kuhusu Afrika kujitoa ICC, Wakuu wa AU wamekubaliana ni mapema mno na itategemea matokeo ya mkutano wa Rome Statue utakaofanyika Nov, 2013.
Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa licha ya makataa hayo kunauwezekano mdogo wa Umoja wa Mataifa UN kukubaliana na maombi haya mapya ya AU kutaka kesi hizo kuahirishwa kwasababu mbalimbali ikiwemo swala la usalama nchini Kenya.
Maazimio ya Umoja was Afrika yanakuja ikiwa imepita miezi kadhaa toka mahakama ya kimataifa ya ICC itupilie mbali ombi la umoja wa Afrika kutaka kesi hizo ziahirishwe kwa madai zinawalenga viongozi wa Afrika pekee.
Katika hatua nyingine hii leo, serikali ya kenya kupitia kwa waziri wake wa mambo ya kigeni inatarajiwa kutoa msimamo wake iwapo itatekeleza maazimio ya Umoja wa Afrika ambayo yanaitaka nchi hiyo kutoshirikiana na mahakama ya ICC na viongozi wake kutohudhuria vikao vya kesi zao.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu na utawala bora yameonya kuhusu hatua ya Umoja wa Afrika kutaka kujiondoa kwenye mkataba wa Roma na sasa wanasubiri kuona athari zitakazotokana hatua ambayo itafikiwa na nchi ya Kenya.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi