MICHUANO ya soka ya Ligi Kuu England, imedhihirisha kuwa na wakali wanaotisha kwa kutikisa nyavu baada ya nyota wake kuwafunika wakali wa ligi za nchi nyingine wakati walipokuwa wakizitumikia timu zao za taifa kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia zilizofanyika Ijumaa iliyopita.
Kwenye mechi hizo za kufuzu upande wa Ulaya,
wakali wa kutoka Ligi Kuu England walifunga mabao 24, karibu mara mbili
ya idadi ya mabao yaliyofungwa na wachezaji wa kutoka kwenye ligi
nyingine kubwa barani humo.
Kwenye orodha hiyo, Arsenal, imeongoza kwa wakali
wake kufunga mabao matano na kufuatiwa na wa Manchester United
walioshinda mabao manne na wa Manchester City mabao matatu.
Kwa idadi ya mabao yote 100 yaliyofungwa siku
hiyo, Ligi Kuu England imechangia karibu robo ya mabao hayo, wakati
inayoshika nafasi ya pili ni Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga’
iliyochangia mabao tisa.
Ligi Kuu Hispania imefunga mabao manane, Ligi Kuu
Ufaransa mabao saba, wakati Ligi Kuu Italia imeambulia mabao manne,
idadi ya bao moja zaidi ya yale yaliyofungwa na wachezaji wa kutoka
kwenye Championship ya England.
Nyota wa Arsenal waliochana nyavu ni Nicklas
Bendtner (mawili), Mesut Ozil na Olivier Giroud (mawili), wakati
Manchester United imeng’ara kupitia Wayne Rooney na Robin van Persie,
aliyefunga mabao matatu.
Manchester City mabao yake yalifungwa na Edin Dzeko (mawili) na Alvaro Negredo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!