KLABU ya Liverpool imeripotiwa kuanza kujiandaa na maisha bila ya straika wake, Luis Suarez, kwa sababu haitasita kumuuza Januari mwakani kama atahitaji kuondoka.
Straika huyo wa kimataifa wa Uruguay anayetajwa
kuwa na thamani ya Pauni 50 milioni, kwenye uhamisho wa majira ya joto
alikuwa akifukuziwa na Arsenal, lakini Liverpool iligoma kumuuza.
Lakini staa huyo aliyemaliza adhabu ya kufungiwa
mechi 10 hivi karibuni iliyotokana na kosa la kumng’ata beki wa Chelsea,
Branislav Ivanovic, amewaambia marafiki zake kwamba anataka kuamsha
mpango mpya wa kuondoka Anfield wakati dirisha dogo la usajili wa
Januari litakapofunguliwa.
Mshambuliaji huyo, mwenye umri wa miaka 26
alimwambia rafiki yake kwamba anataka kuondoka Liverpool na kwenda
kujiunga na klabu ambayo itashindania mataji makubwa ikiwamo Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Arsenal inatazamiwa kurudi na ofa yake ya kumnasa
straika huyo, lakini ripoti zinabainisha kwamba straika huyo hatakubali
kwenda Emirates kama miamba ya Hispania, Real Madrid itaingia kwenye
mchakato wa kuhitaji saini yake.
Liverpool imedaiwa kwamba haitakuwa tayari
kuendelea kupambana kumbakiza mchezaji huyo kama atahitaji kuhama kama
alivyodai kwenye uhamisho wa majira ya kiangazi mwaka huu.
Suarez amewaambia marafiki zake wa karibu kwamba ataendelea kuboresha kiwango chake cha sasa ili kuzivutia timu kubwa.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!