KIPA
wa zamani wa Liverpool, Charles Itandje amefanya zi nzuri jana kuisaidia
Cameroon kulazimisha sare ya 0-0 ugenini na Tunisia katika mechi ya
kwanza ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia, hatua ya mwisho.
Baada
ya kupewa nafasi ya pili kufuatia Cape Verde kuondolewa, Watunisia
walishamulia sana dakika za mwanzoni, lakini wakakwamishwa na mlinda
mlango mwenye umri wa miaka 30 mzaliwa wa Ufaransa.Nahodha wa Cameroon, Samuel Eto'o, alirejea uwanjani jana baada ya kustaafu kwa muda mfupi na alikuwa mwiba mkali kwa safu ya ulinzi ya Tunisia katika mechi hiyo ya kusaka tiketi ya Brazil mwakani.
Timu hizo zitarudiana mjini Yaounde Novemba 17 na mshindi atakwenda Brazil.
Katika mchezo mwingine jana, mabao mawili ya Emmanuel Emenike yameipa Nigeria ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Ethiopia, iliyotangulia kupata bao baada ya kipa na Nahodha wa Super Eagle, Vincent Enyeama kuipangulia nyavuni krosi ya Behailu Assefa.
Katika mechi za juzi, Burkina Faso ilishinda 3-2 nyumbani dhidi ya Algeria, wakati Ivory Coast ilishinda 3-1 nyumbani dhidi ya Senegal. Ghana itamenyana na Misri Jumanne.


0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!