WAKATI washambuliaji wa kocha, Jose Mourinho, katika klabu ya Chelsea wakiwa wamekaukiwa mabao, inashangaza kuona kocha huyo amemtoa kwa mkopo staa wake wa Ubelgiji, Romelu Lukaku, ambaye anafunga kadri anavyojisikia katika klabu ya Everton.
Pia Lukaku ameipeleka Ubelgiji katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil. Ni nani huyu Lukaku.
Azaliwa Ubelgiji, baba yake mwanasoka Congo
Lukaku alizaliwa katika Jiji la Antwerp, Kaskazini
mwa Ubelgiji huku baba yake akiwa ni Roger Lukaku ambaye ni staa wa
zamani timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Mdogo
wake, Jordan yupo katika timu ya vijana ya Anderlecht ambayo Lukaku
alipitia.
Lukaku alianza kucheza soka katika umri wa miaka
mitano katika klabu ya Rupel Boom kabla ya kuonwa na maskauti wa klabu
ya Lierse SK.
Aliichezea kuanzia mwaka 2004 hadi 2006 akifunga
mabao 121 katika mechi 68. Baadaye akajiunga na timu ya vijana ya
Anderlecht, akiifungia mabao 131 katika mechi 93.
Atua Anderlecht, Chelsea yamwona
Lukaku alisaini mkataba wa kulipwa na Anderlecht
mnamo Mei 13, 2009 akiwa na umri wa miaka 16 na siku 11 baadaye
aliichezea timu hiyo katika mechi dhidi ya Standard Liège. Kuanzia
wakati huo, maskauti wa Chelsea walikuwa wakimfukuzia kwa kasi.
Amfuata shujaa wake Didier Drogba
Agosti 2011, Lukaku alijiunga na Chelsea kwa ada
ya Pauni 12 Milioni ambayo ingeongezeka mpaka kufikia Pauni 17 Milioni
kutokana na kiwango chake.
Alipewa jezi namba 18 na kwa kufanya hivyo alikuwa
ametimiza ndoto zake za kukipiga na mshambuliaji Didier Drogba ambaye
anamtaja kama shujaa wake wa maisha ya soka.
Mechi yake ya kwanza alicheza dhidi ya Norwich akiingia uwanjani kuchukua nafasi ya Fernando Torres.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!