Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KITENDO CHA M23 KUISHAMBULIA NDEGE YA MAJESHI YA MONUSCO UN YAKILAANI

KITENDO CHA M23 KUISHAMBULIA NDEGE YA MAJESHI YA MONUSCO UN YAKILAANI

Written By Unknown on Saturday, 19 October 2013 | Saturday, October 19, 2013

Umoja wa Mataifa nchini DRCongo, umelituhumu kundi la waasi wa M23 kushambulia helikopta yake hapo jana, ikiwa ni tukio la pili katika kipindi cha juma moja. Duru za Umoja wa Mtaifa nchini DRCongo zimearifu kwamba helikopta mbili za monusco zilizokuwa katika shughuli za kupiga doria, moja ilishambuliwa na makombora yaliorushwa na waasi wa M23.

Mjumbe wa umoja wa Mataifa nchini DRCongo Martin Kobler pamoja na mjumbe maalum wa Umoja huo katika ukanda wa maziwa makuu Bi Merry Robinson wamelaani vikali kitendo hicho cha kushambulia helikopta ambayo ilikuwa haina silaha, ikiwa na tukio lapili kwa kipindi cha juma moja.
Wajumbe hao wa Umoja wa Mataifa walikuwa jana jijini Kampala nchini Uganda kuiga jeki mazungumzo ya kusaka amani baina ya serikali ya Drcongo na waasi wa kundi hilo la M23, Mazungumzo ambayo yanapwaya tangu majuma kadhaa.
Katika hatuwa nyingine, raia wa maeneo ya mashariki mwa nchi ya kidemokrasia ya Congo hii leo wanafanya kumbukumbu ya kutekwa kwa makasisiwa kanisa katoliki tangu Octoba 19 mwaka jana na ambo hadi leo wapo mikononi mwa kundi lililowateka.
Shirika la kijadi ambalo limeandaa shughuli za maombelezi hayo limewatolea wito wananchi wa maeneo ya Beni kuvaa nguo nyeusi kuungana na wahanga wote ambao , shirika hilo limesema idadi imefikia zaidi ya mia nane.
Shirika hilo limewatolea wito serikali ya congo Kinshasa, Umoja wa Mataifa, wanasiasa kuingilia kati ili watu hao waweze kuachiwa huru.
Ibada ya misa kuwaombea mateka hao imepangwa kufanyika katika kanisa moja jijini Beni.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi