Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HUENDA MAZUNGUMZO YANAYO ENDELEA KULE MJINI GINIVA KUHUSU IRAN YAKAZAA MATUNDA MAZURI

HUENDA MAZUNGUMZO YANAYO ENDELEA KULE MJINI GINIVA KUHUSU IRAN YAKAZAA MATUNDA MAZURI

Written By Unknown on Wednesday, 16 October 2013 | Wednesday, October 16, 2013

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya EU, Catherine Ashton
Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya
Mazungumzo kati ya mataifa ya magharibi na ujumbe wa Iran yanaingia siku yake ya pili hii leo huku kukiwa na matumaini kuwa huenda safari hii mazungumzo haya yakazaa matunda licha ya ugumu uliopo.

Mazungumzo haya yanayofanyika mjini Giniva Uswis na kusimamiwa na mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya EU, Catherine Ashton ambaye kupitia msemaji wake anasema kuna matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano kuhusu baadhi ya mapendekezo kuhusu mapngo wa nyukilia wa Iran.
Kwa upande wake nchi ya Iran kupitia kwa naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, Abbass Aragachi anasema kuwa nchi yake haikuja kwenye mazungumzo haya kama watalii na kwamba wamejidhatiti kushirikiana na jumuiya ya kimataifa huku akishindwa kueleza undani wa mapendekezo yao mapya.
Viongozi kutoka Mataifa yenye nguvu duniani kwa siku ya pili wamekuwa na mazungumzo mjini Geneva Uswis juu ya nchi ya Iran kuhusu mpango wake wa Nyuklia,Mazungumzo haya ya siku mbili yanatarajiwa kujadili kwa kina mapendekezo yaliyowasilishwa na nchi ya Iran kuhusu mpango wke wa nyuklia na namna inavyopanga kushirikiana na jumuiya ya kimataifa.
Mazungumzo ambayo yanalenga kumaliza tofauti kati ya Iran na jumuiya ya kimataifa jkuhusu mpango wake wa Nyuklia.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi