Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » JAPO KUNA MKANGANYIKO ILA JUHUDI ZA KUWASHAWISHI SYRIA KWELEKEA KWENYE MKUTANO WA PILI WA GENEZA ZIMESHIKA KASI

JAPO KUNA MKANGANYIKO ILA JUHUDI ZA KUWASHAWISHI SYRIA KWELEKEA KWENYE MKUTANO WA PILI WA GENEZA ZIMESHIKA KASI

Written By Unknown on Saturday, 19 October 2013 | Saturday, October 19, 2013

Lakhdar Brahimi makao makuu ya UN Genève
Mpatanishi katika mgogoro wa Syria Lakhtar Brahim anafanya ziara nchini Misri kujadili kuhusu maandalizi ya mkutano wa Geneva ya pili kuhusu Syria, wakati kukiwa hakuna uhakika iwapo mkutano huo utakuwepo kufuatia hali ya mkanganyiko ambayo inaendelea kuukumba mkutano huo.

Hapo jana kiongozi mmoja wa serikali ya Syria alifahamisha kwamba mkutano huo umepangwa kufanyika Novemba 23 ijayo, taarifa iliokanushwa na Urusi na marekani waandalizi wa mkutano huo kufuatia wapinzani wa serikali ya rais Assad kuendelea kutia ngumu ya kushiriki kwenye mazungumzo hayo na haijulikani iwapo mkutano huo utafanyika.
Kwa mujibu wa Serikali ya Urusi na ile ya Marekani waandalizi wa mkutano huo wa Geneva ya pili kuhusu Syria, lengo hasa ni kuandaa mkutano huo mwishoni mwa mwezi Novemba, hata hivo upinzani bado inapinga kushiriki katika mkutano huo .
Mapigano yameshika kasi wakati huu Mpatanishi wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za kiarabu lakhtar Brahimi akianza ziara katika ukanda huu kwa ajili ya kuandaa mkutano huo
katika mji wa A Deir Ezzor mashariki mwa syria, wapiganaji wa makundi ya jihadi wamewanyonga wanajesi kumi wa serikali huku watu zaidi ya kumi wakipoteza maisha kaskazini mwa taifa hilo kufuatia mashambulizi ya anga katika mji wa kikurdi.
Mbali na ziara hiyo ya mpatanishi Lakhtar Brahimi, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry anaanza ziara ya siku kadhaa barani ulaya juma lijalo ili kujadiliana na viongozi wa Ulaya kuhusu mkutano huo wa Geneva.
Saudi Arabia mshirika wa karibu wa makundi ya waasi wa serikali ya Syria, imekataa kuchukuwa kiti chake kwenye baraza la Uslama la Umoja wa Mataifa, ikiituhumu Umoja huo kushindwa kuupatishia suluhusu mgogoro wa Syria.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi