LIVERPOOL kwa sasa ni kali, mtu akibisha anakuwa jeuri tu.Inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi saba unawezaje kusema siyo wakali?
Hata hivyo ukali wa kikosi hicho kwa sasa
umechangiwa na juhudi kubwa na ushirikiano kati ya mastraika Daniel
Sturridge na Luis Suarez.
Ushirikiano wa wachezaji hao msimu huu
umewashangaza wapenzi wengi wa soka. Mbio, maarifa, kumiliki mpira kwa
muda mrefu na kutikisa vyavu ni baadhi ya sifa za wachezaji hao msimu
huu.
Kiwango chao kimefanya wafunge jumla ya mabao 11
mpaka sasa. Wachezaji hao wamepewa jina la pamoja la S.A.S, hapo
mashabiki wanakumbuka wachananyavu wa siku za nyuma wa Blackburn
Rovers, Alan Shearer na Chris Sutton.
Kwa sasa mashabiki wanashangilia, angalau
wamefutwa machozi ambayo yamekuwa yakiwatoka kwa misimu kadhaa. Lakini,
mashabiki wa klabu hiyo watacheka kwa muda mrefu? Jibu ni hapana, kwa
sababu ushirikiano wa wachezaji hao unaweza kuvunjika wakati wowote.
Hebu tuone sababu za Liverpool kutokushangilia sana ikiwa na wakali hao waliopachikwa jina ka S.A.S.
Suarez mguu ndani nje
Liverpool wamefurahia juhudi za klabu kumbakiza
Suarez, wakati mchezaji huyo alipotaka kuondoka, lakini wafahamu kuwa
lengo la nyota huyo wa Uruguay lipo palepale, anasubiri dirisha lingine
la usajili ili aanzishe sokomoko jipya.
Mchezaji huyo amesema kocha wake hamwamini sana na
haoni sababu ya kuendelea kucheza ligi ambayo vyombo vya habari
vinammulika yeye tu uwanjani.
Mchezaji huyo aliwahi kuongeza kuwa anataka
kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na si vinginevyo. Lakini nani anaweza
kumlaumu. Suarez kwa sasa ana umri wa miaka 26 na muda wa kucheza
umeanza kumtupa mkono taratibu, anahitaji kutimiza malengo yake.
Suarez alishawahi kusema hawezi kukataa kuhamia
kwenye klabu kubwa kama Real Madrid au Bayern Munich. Kipaji cha Suarez
kinatosha kupata ubingwa wowote, lakini akiwa na Liverpool, nafasi yake
inakuwa finyu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!