Klabu ya
soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo Jumamosi
itamenyana na klabu ya Stade Malien katika mchuano wa nusu fainali ya
pili kuwania taji la shirikisho barani Afrika.
Mchuano huo utachezwa mjini Lumbumbashi kuanzia saa kumi na
nusu saa za Afrika ya Ktai mchuano ambayop TP Mazembe watakuwa dimbani
wakiwa wanaongoza kwa mabao 2 kwa 1 kutokana na ushindfi wao wa mzunguo
wa kwanza wiki mbili zilizopita.
Hata hivyo, gumzo kubwa mjini lubumbashi kwa sasa ni kukosekana kwa wachezaji wa Zambia wanaoichezea timu hiyo Rainford Kalaba, Stoppila Sunzu na Nathan Sinkala baada ya serikali ya Lusaka kuwazuaia kurudi DRC kuichezea klabu yao.
Serikali ya Zambia ilitoa agizo la kukamatwa kwa wachezaji hao baada ya kutoichezea timu yao ya taifa katika mchuano wa kirafiki wa kitaifa dhidi ya Brazil katikatika ya mwezi huu.

. |
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!